Terms and Conditions

Swahili

Vigezo na Masharti ya Kutumia Mtandao wa JamiiDeals

Mnunuzi/Mteja

1. Taarifa zako utakazo tupatia mfano namba ya simu,barua pepe,jina lako n.k tutazitumia katika kuboresha huduma zetu mfano kupokea jumbe mbalimbali moja kwa moja kwa SMS n.k

2. Endapo utafanya malipo kwa njia ya Xtreem Pay, JamiiDeals itakusaidia endapo unahitaji kurudisha mzigo uliopokea (kama unatatizo) kutoka kwa muuzaji yoyote au kurudisha salio lako, Endapo utamlipa muuzaji kwa njia ya pesa taslimu au njia nyingine yoyote tofauti na Xtreem Pay, JamiiDeals haitahusika katika kukurudishia pesa au kubadilishiwa mzigo itabidi muelewane na muuzaji moja kwa moja. Muda rasmi ambao mnunuzi anaweza kurudisha bidhaa au salio la Xtreem Pay ni siku 7 toka afanye malipo ya Oda husika kwa Xtreem Pay.

3. Endapo itagundulika akaunti yako inajihusisha na utapeli au uvunjaji wa sheria, Akaunti yako itafungwa.

 

 

Muuzaji

1. Kwa wauzaji wa Akaunti 'A' au Akaunti ya kwanza, Kila muuzaji atatakiwa kilipia TZS 20,000 kila mwezi endapo anahitaji duka lake liendelee kuwepo JamiiDeals. JamiiDeals itachukua ada (commision) ya asilimia kumi (10%) ya malipo ya Order(ukitoa pesa ya Delivery). 

2. Kwa wauzaji wa Akaunti 'B' au Akaunti ya pili, Kila muuzaji atatakiwa kilipia TZS 50,000 kila mwezi endapo anahitaji duka lake liendelee kuwepo JamiiDeals. JamiiDeals haitachukua ada (commission) kwa wauzaji wa Akaunti B.

3. Kwa Order zilizolipiwa kwa Xtreem Pay, JamiiDeals itamlimpa pesa muuzaji kwa njia za Mobile Money (mf. tigopesa,mpesa,airtel money n.k kwa sasa) wiki moja baada ya order husika kulipiwa. Ndani ya hiyo wiki mnunuzi anauwezo wa kuomba kurudisha bidhaa au kubadilishiwa endapo bidhaa itakua sio halisi,imekosewa,inamatatizo n.k Endapo bidhaa itaombwa kurudishwa, Pesa ya Muuzaji itashikiliwa kwanza mpaka mgogoro utakapoisha na mnunuzi au muuzaji atakapo thibitisha.

4. Bidhaa zote ambazo muuzaji atauza ni lazima ziwe mpya (hazijatumika popote) na halisi (original), Endapo itathibitika muuzaji unauza bidhaa zisizo mpya au halisi akaunti yako itafungwa na hautorudishiwa pesa ya ada ya kila mwezi au pesa itakayosalia ya Order zilizolipwa kwa Xtreem Pay.

5. JamiiDeals itatoa elimu kwa wauzaji ya namna ya kuweka bidhaa kwenye mtandao na picha/video zinazostahili. JamiiDeals inahaki ya kuifuta bidhaa husika endapo itakua haijakidhi vigezo vya ubora wa picha / video vinavyostahili au maelezo yasiyojitosheleza.

Vigezo hivi na Masharti haya yamehaririwa mara ya mwisho Tarehe 22 Oktoba 2022.

About Company

Contact Us

FAQ

Top